Header Ads

MKEMIA MKUU AKANUSHA DAI LA KUCHAKACHUA MATOKEO DAWA ZA KULEVYA


MTAALAMU Mwandamizi katika Idara ya Dawa za Kulevya katika ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Zanzibar, Khamis Rashid Kheir amesema, idara hiyo inafanya kazi kwa uadilifu na haichakachui matokeo ya vipimo kama inavyodaiwa na baadhi ya wananchi.

Akizungumza na Nipashe, Kheir alisema kuwa baadhi ya wanajamii wamejenga dhana kuwa ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali imekuwa ikibadilisha matokeo baada ya kufanya uchunguzi jambo ambalo sio sahihi.

Kheir alizungumza na Nipashe katika maonesho ya biashara yanayoendelea kwenye viwanja vya Maisara mjini Zanzibar.

Alisema malalamiko hayo yanatolewa na baadhi ya wanajamii hasa katika kesi za dawa za kulevya, hivyo ametaka watu kuondokana na dhana hiyo ambayo ni "potofu".

“Tumekuwa tukipata malalamiko kuwa tunabadilisha matokeo hasa katika dawa za kulevya, (lakini) sisi tunapofanya uchunguzi tunatoa taarifa sahihi,”alisema mtaalamu huyo.

Aidha, Kheir alisema kuanzishwa kwa Sheria ya Udhibiti wa Kemikali kumepunguza matumizi mabaya ya kemikali.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!