Header Ads

MBUNGE WA KAHAMA JUMANNE KISHIMBA ATOA ZAIDI YA SHILINGI MIL 53 ZA MFUKO WA JIMBO KUSAIDIA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA.

 ZAIDI ya Shilingi  Milioni 53,000,000 za Mfuko wwa jimbo la Kahama  Mjini zinatarajia kutumika kwaajili ya kusaidia ujenzi wa Vyumba vya madarasa  katika shule mbalimbali za msingi na Sekondari  katika Jimbo hilo mkoani Shinyanga.

Aidha Fedha hizo pia zitatumika katika   kukabiliana na tataizo la upungufu wa matundu yya choo katika baadhi ya shule ambazo zinauhitaji wa matundu  ya Choo na kwamba fedha hizo zinaweza kununua matofali  50,000.

Mbunge wa jimbo hilo, Jumanne Kishimba, akizungumza jana na Wenyeviti wa serikali za mitaa na vijiji na kamati za shule alisema  fedha hizo tayari zimeanza kutolewa katika shule hizo ambapo fedha hizo zinagawiwa kulingana  na mahitaji ya shule.

Kishimba aliiwataka Wenyeviti wa serikali za Mitaa na Vijiji kuwa wasimamizi wakubwa katika Miradi hiyo ya Shule ili kuhakikisha tatizo la Upungufu wa  vyumba vya madarasa katika  halmashauri ya mji wa Kahama/Jimbo la Kahama mjini linapungua kwa muda mwafaka.

Nao Viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Kamati za shule wamempongeza mbunge  huyo kwa kuelekeza nguvu katika kutatua tatizo la vyumba vya madarasa katika shule ningi za jimbo hilo na kuomba kusaidia kusukuma upatikanaji wa vibali vya michango ili wananchi nao washirikishwe.

Halmashauri ya Mji wa Kahama  ambapo ndipo Jimbo la Kahama mjini linapatikana  ni miongoni mwa halmashauri nchini zinazokabiliwa na tataizo la Upungufu wav yumba vya madarasa na  matundu vya vyoo kutokana na kuandikisha idadi kubwa ya wanafunzi kuingia darasa la awali,la kwanza na kidato cha kwanza mwaka huu.

Kwa Mujibu wa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji wa Kahama, Anderson Musumba, Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyangaa  inatarajia kuandikisha zaidi ya wanafunzi 29,000 kwaajili ya  kuanza masomo yao mwaka huu  katika ngazi ya elimu  ya Msingi na sekondari.

Wanafunzi  25,300      ni wale wanaotarajia kuanza masomo ya darasa la awali na la kwanza  huku wanafunzi  4602 nao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza  mwaka huu katika  sule za sekondari za halmashauri hiyo.

Hata hivyo MSUMBA amesema kutokana na ongezeko la uandikishaji wanafunzi mwaka huu, Halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu wa vyumba vya madarasa  1,300 na madawati 4,700 kwa shule za msingi na upande wa sekondari ni  vyumba vya madarasa  102.


 MATUKIO KATIKA PICHA:
 WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA NA BAADHI YA WENYEVITI WA BODI YA SHULE WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI MBUNGE KISHIMBA HAYUPO PICHANI.

 WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAAGIZO YA MBUNGE KISHIMBA.

 KIKAO KIKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI KAHAMA

 KATIBU WA MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA MJINI MR ABDUL AKITOA MAELEZO KWA WENYEVITI WA MITAA KUHUSU NAMNA WATAKAVYOZIPATA PESA KWA AJILI YA KUANZA UJENZI.

 MWENYEKITI WA WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA AKITOA MAELEZO KWA WAJUMBE WA MKUTANO.

 MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA MJINI JUMANNE KISHIMBA AKIWASIKILIZA KWA MAKINI WENYEVITI WA SERIKALI ZA MITAA.
 
 KIKAO KIKIENDELEA KATIKA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MJI WA KAHAMA.

 MBUNGE WA JIMBO LA KAHAMA MJINI JUMANNE KISHIMBA AKIHITIMISHA KIKAO


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!