Header Ads

MBUNGE HAONGA AFICHUA KUWA WABUNGE WANAJIUZA

Mbunge wa Jimbo la Mbozi Mkoani Songwe kwa tiketi ya (CHADEMA), Pascal Haonga amefunguka na kusema kuwa baadhi ya wabunge wamekuwa wakijiuza na kununuliwa kwa bei ndogo na kudai yeye hawezi kuwa sehemu ya watu hao ambao wananunuliwa.

Haonga amesema hayo alipokuwa akifanya mkutano wa hadhara na wananchi wa jimbo lake la Mbozi na kusema wabunge na wanasiasa ambao wana hama vyama kwa kununuliwa na kujidai wanaunga mkono utendaji wa Rais wana upungufu wa akili.

"Mimi siwezi kufanya kama wabunge wengine huko ambao wamekua wakijiuza kwa bei ndogo, mmesikia madiwani wananunuliwa, wabunge wananunuliwa. Hivi inangia akilini kweli wananchi walikuchagua na wengine walichoma nyumba za wengine, wengine waliamua kuchoma na magari, wengine waliamua kuchoma na mahakama, baiskeli na Pikipiki halafu unakuja kusema eti namuunga mtukufu kwa jitihada na kazi anazofanya. Hivi wewe Mbunge utakuwa na akili au matope" alihoji Haonga

Mbali na hilo Mbunge huyo amewaeleza wananchi wake kuwa endapo yeye atarudi CCM basi wachome nyumba zake na mali zake zote na kudai hawezi kurudia matapishi yake.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!