Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MATONYA NAYE ATAKA KWENDA KUONANA NA RAIS MAGUFULI KUMSHUKURU KWA MSAMAHA

Wakati Babu Seya na mwanaye wakiwa tayari wametimiza azima yao ya kumuona Rais, Mganga Matonya, aliyeepushwa kifungo cha maisha, analalamikia hali yake kuwa imemzuia kusafiri kwenda Ikulu kumueleza jambo Rais John Magufuli.

Matonya, ambaye alikuwa mfungwa mwenye umri mkubwa kuliko wote kati ya walioachiwa huru, alikuwa anatumikia kifungo cha maisha baada ya awali kupata msamaha wa adhabu ya kunyongwa kutokana na kupatikana na hatia ya kuua na ameishi gerezani miaka 43.

“Mtakumbuka nilikuwa mtu wa kwanza kati ya tuliotoka gerezani niliyetamka kutaka nimuone Rais, lakini hadi sasa nashindwa kumuona,” alisema Matonya ambaye  siku alipotoka Gerezani alisema ana neno la kumueleza Rais na asipopata nafasi, atakufa nalo.

“Siko tayari kumwambia mtu mwingine zaidi ya Magufuli kipenzi changu,” alisema.

Akizungumza kwa simu kutoka Kijiji cha Wiliko, Matonya alisema taarifa za wanamuziki hao alizipata kutoka kwa mtoto wake na kwamba zilimliza kwani angepata nafasi hiyo kabla hajafa, angejisikia huru katika nafsi yake.

“Alipokuja (Rais Magufuli) kwenye mkutano wa CCM Dodoma niliwaomba watoto wangu wanipeleke. Tatizo wanaona kama nimechanganyikiwa lakini siyo kweli,” alisema Matonya.

Mzee huyo aliomba taasisi na mashirika mengine kumsaidia kumuona Rais Magufuli.

Mtoto wake, Aron alisema aandike ujumbe wake hata magazetini na Rais atauona.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News