Header Ads

MAPACHA WATATU WAPEWA MAJINA YA VIONGOZI WA CHADEMA

Mwanamke mmoja Martha Alphonce Haule mkazi wa Kata ya Nafulala, Sumbawanga mkoani Rukwa amejifungua watoto mapacha watatu na kuwapatia majina ya Halima Mdee (wa kike) pamoja na Mbowe na Lissu (wakiume wawili).

Watoto hao ambao wana mwezi mmoja wamezaliwa kufuatia mwanamke huyo kupata uchungu ghafla baada ya kusikia Mwenyekiti huyo wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA Taifa Mhe. Mdee atazuru Sumbawanga na kutembelea kikundi chao cha Wanawake Tunaweza kilichopo katika Kata ya Mafulala.

Mwenyekiti huyo wa BAWACHA leo tarehe 11 januari 2018 akiwa katika siku ya pili ya ziara yake yenye lengo la ujenzi na uenezi wa chama ikiwa ni pamoja na kuangalia uhai wa baraza hilo na kutoa mwongozo wa shughuli mbalimbali za kichama ametembelea kikundi hicho cha kina Mama na kuwaona watoto hao na pia kama Baraza wamechangia kikundi hicho shilingi 200,000 ikiwa ni ishara ya kuunga juhudi za wanawake hao.

Awali katika ziara hiyo ambayo ameongozana na Katibu wa BAWACHA Taifa Mhe. Grace Tendega, Mjumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA Mhe. Suzani Mgonukulima, Mbunge Viti Maalumu Mhe. Aida Khenan na Viongozi BAWACHA Rukwa walitembelea vikundi vingine vya wanawake vya Sayari, Tupendane (Katandala) na kuweza kuongea nao pamoja na kuchangia fedha kama ishara ya kuunga mkono juhudi za wanawake hao.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!