Header Ads

MAMBOSASA ATOA ONYO KALI KWA WALIOACHIWA NA MAGUFULI


Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, katika matukio tofauti imekamata Silaha hatari aina ya AK 47 mnamo tarehe 7/1/2018 majira ya 10;00 maeneo ya Popobawa, kunawatu wanaomiliki silaha isivyo halali na huenda zinatumika katika matukio mbalimbali ya uny'ang'anyi wa kutumia silaha.

Askari waliweka mtego na kufika eneo hilo Nyumbani kwa Mzee Said Omary [62] na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wakiwa na silaha hiyoaina ya AK 47 yenye namba UC 49331998 ambayo haikuwa na magazine yake.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Ally Makwaya [40] mkazi wa Tandale kwa Tumbo, katika mahojiano kuhusu wapi waliipata silaha hiyo walieleza kuwa shughuli zao kubwa ni kuokota makopo na vyuma chakavu na kuwa hata silaha hiyo waliokota huko eneo la karakana [garage] Kinondoni Mwinyijuma.

Pia katika tukio lingine wamekamatwa watuhumiwa nane kwa makosa ya uhalifu Jijini Dar es Salaam pamoja na vielelezo mbalimbali .

 Jeshi la Polisi Kanda maalum mnamo tarehe 3/1/2018 majira ya saa 3: 30 huko maeneo ya Sinza karibu na kituo cha kuuza Mafuta BIG BON lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili Abdulkareem Bashir [24] , Emmanuel John Bundala [22] mwanafunzi wa VETA mwaka wa tatu kwa kujihusisha na matukio ya wizi wa Magari, vifaa vya magari na wizi katika Benki kwa kutumia Master Cards na Master Keys.

Watuhumiwa hao walipokamatwa walikutwa na vielelezo ambavyo ni Radio Call moja aina ya Redwlls, kadi kumi za benki mbalimbali zikiwemo Tembo card Master card, Leseni mbili za udereva, Funguo malaya 15 ambayo hutumia kwenye matukio ya wizi na Smartphone moja nyeusi.

katika mahojiano watuhumiwa hao wamekiri katika matukio mbalimbali ya wizi huko Mabibo na Sinza na kuonyesha magari mawili yanayodhaniwa kuwa ni ya wizi pamoja na Pikipiki moja

Aidha kwenye tukio lengine jumla ya watuhumiwa sita walikamatwa wakiwa na vielelezo mbalimbali Runinga nane, Redio moja ya Samsung na spika nne vilivyokuwa vimefichwa Nyumbani kwa mtuhumiwa mmoja wapo.

Hatahivyo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam mnamo tarehe 23/12/2017 majira ya saa 09:50 lilifanikiwa kuwakamata majambazi wawili wanaojihusisha katika matukio mbalimbali ya uhalifu ikiwemo uny'ang'anyi wa kutumia silaha pamoja na uvunjaji wa Nyumba na majengo mbalimbali.

Watuhumiwa hao ni Abdallah Iddy [22] na Edward Charles [24], ambapo walikamatwa na Coking Handle pamoja na mtambo wa bunduki inayosadikika kuwa ni shotgun.

Baada ya mahojiano makali na watuhumiwa hao waliweza kuonyesha Nyumba moja iliyopo Kitunda  Nyangasa inayomilikiwa na mtu aitwaye Wally Kimaro ambaye kwa sasa hajulikani alipo

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!