Header Ads

MAKONDA AWATANGAZIA MKUTANO WAMILIKI WA SHOWROOM ZA MAGARI JIJINI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda anawatangazia kuwa atakuwa na mkutano na wafanyabiashara na wamiliki wa showroom za magari wanaofanya shughuli zao hapa jijini siku ya jumatano tarehe 17/01/2018 katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa,Boma Ilala, kuanzia saa nne kamili asubuhi.
Ewe mfanyabiashara wa magari na mmiliki wa showroom,mkutano huu sio wa kukosa kwani mambo mbali mbali ya mustakabadhi wa maswala ya biashara ya magari yatajadiliwa na kupatiwa ufumbuzi huku maazimio mema yakiwekwa kushirikiana na serikali yako ya Mkoa wa Dar es salaam.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!