Header Ads

KUTANA NA PAMPU HIZI ZA KUKAMUA MAZIWA NA KUYAHIFADHI MWANAMKE AKIWA SAFARINI

Pampu za kukama maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini
Kampuni mbili zimetengeneza pampu ambazo zitawasaidia wanawake wanaonyonyesha kukama maziwa na kuyahifadhi wakati wakiwa safarini.
Wanawake wanaotumia pampu kawaida hukamua maziwa mara kwa mara kwa siku na kati ya muda wa dakika 20.
Kwa kawaida huunganishwa kwa stima na hutoa sauti.
Kampuni za Willow na Freemie Libert zimetangenezwa kwa njia ambazo zitakuwa rahisi kuvaliwa.Pampu za kukamua maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini
Kinyume na za zamani, za sasa hutumia betri na hazina sauti.
Zote ziko kwa maonyesho ya CES ya biashara huko Las Vegas.
Willow ilishinda tuzo kutokana na kifaa hicho kwenye maonyesho ya CES mwaka 2017, kwa sababu pampu hiyo imekuwepo kwa majaribio lakini sasa inaingia rasmi sokoni kwa dola 479.
Hata hivyo imekosolewa mitandaoni kutoka kwa wale wameijaribu wengine wakesema kuwa mifuko hiyo ya maziwa ni midogo mno.Pampu za kukama maziwa na kuyahifadhi mwanamke akiwa safarini

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!