Header Ads

KAULI YA ZARI KUHUSU DIAMOND KUFUNGUA KITUO CHA REDIO NA TV

Mama watoto  wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady amempongeza muimbaji huyo mara baada ya kuweka wazi ujio wa kituo chake cha redio na runinga.

Katika pongezi hizo Zari amemtaja Diamond kama mtu anayejituma zaidi katika kile anachokifanya. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Zari ameandika;

Hongera Damond Patnumz sana kwa juhudi na bidii uliyonayo Allaah akujalie kwa mengine mazuri zaidi. Siku zote umekuwa mpiganaji wa kazi zako, kwa kuwa njia pekee ya kuijenga familia ni kupiga KAZI najua malengo yako Alhamdulillah! #wcbTV #wcbFILMSTUDIO #wcbMUSICSTUDIO #wcbRADIO #wcbHEADQUATERS.

Bila kusahau #DiamondKaranga na chibuperfume #ChibuPerfume 2018 looking good👌🙏

Hapo jana Diamond aliachia video mtandaoni ikionyesha mjengo mpya wa WCB ambao utatumika kama makao makuu ya kampuni hiyo pamoja na studio za Wasafi TV na Wasafi Redio. 
Pia utakumbuka hii si biashara ya kwanza kwa Diamond kwani ameshaingiza sokoni manukato yake ‘Chibu Perfume’ pamoja na Karanga.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!