Header Ads

HOFU YATANDA BOMBA LA GESI KUPITA UWANJA WA NDEGE

Bomba la kusafirisha gesi asilia kutoka mkoani Mtwara kwenda jijini Dar es salaam limeanza kuleta utata baada ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege(TAA) kulihofia kutokana na kupita uwanja wa ndege.

Bomba hilo linapita katika hifadhi ya Uwanja wa Ndege wa Mtwara ambao uko katika mpango wa kuupanua ili kuendana na mahitaji ya usafiri wa anga  baada ya TAA kuanza utaratibu wa kuupanua uwanja huo.

Hayo yamebainika baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa kutembelea uwanja huo na kuliagiza Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) pamoja na TAA kukaa na kuona ni kwa namna gani wataliondoa bomba hilo ambalo limeonekana kukwamisha shughuli za upanuzi wa uwanja.

“Kama nilivyosema hii haiwezi kukubalika, nirudie kusema TPDC na TAA na wataalamu wa wizara waje wakae lakini kikubwa waangalie namna ya kulitoa hili bomba kwa sababu hizi ndege zitakapokuwa zikishuka hapa wanaweza kufuta safari zake  wakigundua kuna bomba la gesi na mimi ninavyojua bomba hili ni hatari,” amesema Kwandikwa

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Uwanja wa Ndege Mtwara, Daimon Mwakosya amesema katika mradi wa kupanua kiwanja hicho na kufikia code 4E na kuwa na uwezo wa kuhudumia ndege aina ya A340-200 na familia hiyo pamoja na Fire Cat 8.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!