Header Ads

ALMASI YA TANO KIUKUBWA YAGUNDULIWA HUKO KUSINI MWA AFRIKA

picha ya mtandao

Leo kampuni ya madini iliopo jijini London imetangaza ugunduzi wa almasi ambayo ina karati
910 na kuifanya almasi ya tano kiukubwa.Almasi hiyo iliyo patikana katika mgodi mdogo wa Lesotho, Afrika Kusini ni nusu ya ukubwa wa moyo wa kiume wa binadamu.

Kutokana na Gazeti la “New York Times” inaripoti kwamba kampuni ya Diamond Gems iligundua Almasi hiyo katika mgodi wa Letseng iliyopo Afrika Kusini na inasemekana kwamba Almasi hiyo haina rangi wala uchafu wowote ambao ungepunguza ukubwa wake.

Serikali ya Lesotho inamiliki sehemu ndogo katika mgodi wa Letseng ambayo inamilikiwa na wadau wengi kutoka British.

Almasi hiyo ndiyo Almasi kubwa zaidi kupatikana katika Leostho nchi ndogo iliyozungukwa na Afrika Kusini. Jiwe ambalo liliweka heshima hadi leo ni Lesotho Promise ambalo lilikuwa na karamu 603 na kuuzwa kwa kiasi cha dola milioni 12.4 kwa mnada zaidi ya miaka kumi iliyopita.

Kwa taarifa zilizotolewa leo ni kwamba Gavana Mkuu wa Gem Clifford Elphick alisema jiwe la hivi karibuni lililogunduliwa ni “exceptional top quality diamond” yaani almasi yenye ubora waki pekee yenye kiwango cha juu zaidi cha rangi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!