Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

ZITTO ARUDI NA HOJA YA UWANJA WA CHATO

Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa ACT Wazalendo, Mhe. Zitto Kabwe amefunguka na kusema kuwa fedha ambazo zimelipwa kwa mkandarasi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato na ununuzi wa ndege za Bombardier na Boeing hazikuidhinisha na CAG.

Zitto Kabwe amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari na kuelezea Maazimio ya Kamati kuu ya ACT Wazalendo kuhusiana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kwa sasa.

"Serikali ilipata gawio la shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kutokana na faida ya benki hiyo mwaka 2015/16. Taarifa juu ya gawio hilo inapatikana katika wavuti ya BOT. Kinyume na utaratibu, Serikali haikutoa taarifa juu ya gawio hili popote kwenye taarifa zake za kiFedha.

"Mapato haya hayakupelekwa Bungeni kugawiwa kwa mujibu wa sheria. Taarifa ni kuwa Serikali iliamua kutumia fedha hizi kulipia Mkandarasi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Chato, pamoja na madeni ya ndege za Bombardier na Boeing bila kufuata taratibu za sheria za fedha na bila Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG kuidhinisha kwa mujibu wa Katiba" alisema Zitto Kabwe

Zitto Kabwe aliendelea kuelezea kuwa "Utaratibu unataka fedha kuingia kwenye Mfuko Mkuu (Consolidated Fund) na kisha kuidhinishwa na CAG, na ndipo Serikali kuanza kutumia. Shilingi bilioni 300 kutumika na Serikali bila kushirikisha Bunge na kufuata sheria za nchi ni kusigina Katiba na kudharau Taasisi za Uwajibikaji za nchi"

Aidha Kamati Kuu wa ACT Wazalendo imemtaka CAG afanye ukaguzi maalum wa fedha hizo na kutoa taarifa kwa Bunge ili sasa Bunge liweze kuiwajibisha na kuisimamia Serikali vizuri.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News