Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

UJIO WA WAZIRI UMMY MWALIMU MSALALA,WAZEE 300 WAULA WAPEWA BURE BIMA YA AFYA YA JAMII.


 WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO UMMY MWALIMU AKIONGEA NA WANANCHI WA MSALALA.


 KAHAMA
Zaidi ya Wazee 300 katika Kata ya Segese Halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga leo wamepatiwa bure Bima ya Afya ya Jamii iliyoboreshwa lengo likiwa ni kuwapatia Wazee hao huduma za Afya bure na kwa wakati.

Akizungumza katika Hafla ya kukabidhi bima hizo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto UMMY MWALIMU amesema serikali haitavumilia kuona mgonjwa mwenye Bima ya Afya akitakiwa alipie matibabu na vipimo.

Waziri MWALIMU ameongeza kuwa serikali inatarajia kupeleka mswaada wa sheria bungeni unaowataka Wananchi wote kuwa na Bima ya Afya na kusema kuwa Bima itakuwa ni suala la lazima na si la hiari kama ilivyo sasa.

Kwa upande wao baadhi ya Wazee wanufaika wa bima hiyo, BERITA MABULA na MIKAELI MACHEBULILA wamesema kuwa bima hizo zitawasaidia kupata matibabu na vipimo kwa haraka tofauti na ilivyokuwa awali.
Waziri MWALIMU ambaye alikuwa katika ziara ya siku moja ya Halmashauri ya Mslala kutathimini jinsi mfumo wa malipo kwa ufanisi RBF unavyofanya kazi amekamilisha ziara hiyo.


 MATUKIO KATIKA PICHA:
 WAZIRI UMMY MWALIMU AKIWA KATIKA MOJA YA KITUO CHA AFYA MSALALA AKIKAGUA CHUMBA CHA KUHIFADHIA DAWA.
 WAZIRI UMMY MWALIMU AKIENDELEA NA ZIARA YAKE KATIKA HALMASHAURI YA MSALALA.
 MMOJA WA WAKAZI WA SEGESE AKITOA MAELEZO MBELE YA WZIRI UMMY KUHUSU HUDUMA ZA AFYA KWA MFUMO WA CHF.
 MMOJA WA WAZEE WALIOPATA NAFASI YA KUANDIKISHWA BURE KWENYE MFUKO WA BIMA YA AFYA JAMII
KIKOSI YA CHA NGOMA YA ASILI KIKITUMBUIZA MBELE YA WAZIRI UMMY MWALIMU.
WAZIRI UMMY MWALIMU AKIWA NA VIONGOZI WA MKOA NA WILAYA WAKIKAGUA MIRADI YA AFYA KATIKA HALMASHAURI YA MSALALA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News