Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

HALMASHAURI WILAYANI KAHAMA ZATAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA MANUNUZI ILI KUEPUKA KUPATA HATI CHAFU.Wahandisi pamoja na viongozi wa halmashauri wilayani Kahama wametakiwa kuzingatia taratibu za manunuzi ili kuziepusha halmashauri zao kupata hati chafu.

Wito huo umetolewa jana na Naibu waziri ofisi ya Rais (TAMISEMI) GEORGE KAKUNDA wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya Ushetu baada ya kukagua miradi ya maendeleo ya halmashauri hiyo likiwemo jengo la muda la utawalala la halmashauri hiyo.

Naibu waziri pia amekagua mradi wa maji katika kijiji cha KAYENZE na kuwataka wahandisi kufanya kazi zao kwa weledi ili kulinda heshima ya taaluma zao.

Wakazi kadha wa kijiji hicho cha KAYENZE wameishukuru halmashauri hiyo kwa kuwaletea huduma ya maji safi na salama na kwamba kabla ya mradi huo wanawake walilazimika kufuata maji umbali mrefu hali inayosababisha ndoa nyingi kuvunjika.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo wa maji mbele ya Naibu Waziri KAKUNDA, Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri ya Ushetu, CHARLES PAMBE amesema mradi huo umegharimu zaidi ya shilingi milioni 837 na unahudumia wakazi zaidi ya 8000 na taasisi sita za umma.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News