Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

GAMBO ATOA NENO KWA WAKUU WA SHULE

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka Wakuu wa shule mbalimmbali mkoani humo kuhakikisha fursa zinagawanywa kwa usawa kwa walimu wote na kutaka dhana ya walimu wanaojipendekeza tu kwa mkuu wa shule kuwa wanufaika wa fursa hizo inakufa.

Mrisho Gambo ameyasema hayo alipokuwa akiongea na baadhi ya walimu wa shule ya  Embarway Sekondari iliyopo Arusha na kusema kama walimu Wakuu wakifanya utaratibu mzuri itasaidia walimu hao kunufaika na fursa mbalimbali kwa usawa, jambo ambalo litasaidia kuondoa upendeleo.

"Kumekuwepo na malalamiko sehemu zingine kwenye zoezi kama la leo hili la kusimamia mitihani unakuta kila mwaka wanakwenda walimu wale wale rafiki zake Mkuu wa shule, kama wewe kiwango chako cha kujipendekeza ni kidogo wewe utakuwa unasikia kwa wengine tu maana orodha ya walimu wanaokwenda kwenye usimamizi huwa inapagwa na Mkuu wa Shule, maeneo mengine nasikia wanaangalia sana jinsi kama ni mdada akimpa ushirikiano zaidi Mkuu wa Shule huyo dada hakosi lakini tumekuwa tukisisitiza hiyo kazi ya kusimamia mitihani ni kazi ya kila mwalimu" alisema Gambo

Aliendelea kufafanua kuwa "Kwa Mkuu wa shule anayejitambua anapaswa kutengeneza utaratibu mzuri ili kuwe na mzunguko, kila mwalimu mwenye sifa aweze kushiriki kwenye zoezi hilo, haiwezekani ukaenda kila mwaka, unaweza kwenda mwaka huu mwakani akaenda mwingine, baadaye ikafika tena zamu yako. Kwa sababu walimu hawa hawana kazi ya ziada, ofisi zingine wanalipwa masaa ya ziada lakini walimu hawalipwi, mwalimu hana posho, mwalimu hana safari, mwalimu yeye ni mitihani, sensa na kusimamia uchaguzi basi sasa hizo fursa zinapaswa kuwekewa utaratibu mzuri ili kila mmoja anufaike nazo"

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News