Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WATEJA WA CHF WAULA,SERIKALI SASA KUANZISHA MADAWATI MAALUMU KWA AJILI YA KUPATA MATIBABU. MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ZAINAB TELACK AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA KATA YA NYAMILANGANO HALMASHAURI YA USHETU.

KAHAMA
  
SERIKALI mkoani Shinyanga imesema kuwa watumiaji wa mfuko wa afya ya Jamii CHF iliyoboreshwa sasa watapata huduma katika madawati maalumu yatakayotengwa katika zahanati na vituo vyote vya afya ili kurahisha upatikanaji wa matibabu kwa wahusika.

Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi Zainabu Telack katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Nyamilangano halmashauri ya ushetu wilayani Kahama.

Telack amesema kuwa serikali imesikia ombi la wateja wa mfuko wa afya wa CHF na kwamba wameamua kuweka dawati  maalumu la wateja hao ili wapate huduma kwa haraka ikiwa ni pamoja na makabati ya dawa.

Katika hatua nyingine Telack amewataka wananchi kuacha kutumia dawa za miti shamba bila kufanya vipimo na kuwataka wafike hospitali kufanyiwa vipimo kabla hawajatumia dawa za miti shamba na dawa zinginezo.

Naye Meneja wa Mfuko wa Jamii CHF iliyoboreshwa halmashauri ya Ushetu Lucy Kihiyo amesema kuwa changamoto wanayokutana nayo ni wananchi kutoona umuhimu wa kujiunga na mfuko huo kwani hawaoni tofauti ya huduma kati ya mteja wa CHF na mteja wa kawaida.

Kwa mujibu wa Takwimu iliyotolewa katika mkutano huo halmashauri ya ushetu mpaka sasa ina jumla ya wanachama 5422 waliojiunga na mfuko wa Afya ya jamii CHF iliyoboreshwa sawa na asilimia 12.47% ya wakazi wote.

MATUKIO KATIKA PICHA:
 
 MENEJA WA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF HALMASHAURI YA USHETU LUCY KIHIYO AKITOA MAELEZO KWA WANANCHI KUHUSU NAMNA YA KUJIUNGA NA MFUMO HUO.

 BAAADHI YA VIONGOZI WA KATA WILAYA NA MKOA PAMOJA NA WAFANYAKAZI WA MRADI WA TUIMARISHE AFYA (HPSS) WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO.

 WANAFUNZI NAO HAWAKUWA NYUMA KUMSILIZA MKUU WA MKOA HAYUPO PICHANI KUHUSU UMUHIMU WA KUJIUNGA NA MFUKO HUO.

 WAKUU WA IDARA WA HALMASHAURI YA USHETU WAKIPUNGA MKONO KUWASALIMIA WANANCHI.

 MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA USHETU MATOMOLA AKIJIBU MASWALI YA WANANCHI KUHUSU MASWALA MBALI MBALI YA AFYA,ELIMU NA KILIMO.

 MKUU WA MKOA WA SHINYANGA ZAINABU TELACK KUSHOTO PAMOJA NA KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TIMOTH NDANYA WAKISIKILIZA KWA MAKINI MASWALI NA KERO ZA WANANCHI.

 WANANCHI WA KATA YA NYAMILANGANO NA VIJIJI JIRANI WAKIWA KATIKA MKUTANO HUO.

 KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TIMOTH NDANYA AKIMKARIBISHA MKUU WA MKOA KUZUNGUMZA NA WANANCHI.

 BAADHI YA WAANDIKISHAJI WA CHF HALMASHAURI YA USHETU WAKIWA NA WAKUU WA IDARA WAKISIKILIZA KWA MAKINI MAAGIZ YA MKUU WA MKOA.

 MENEJA MKOA WA MRADI WA TUIMRISHE AFYA (HPSS) DR HARUN KASALE ALIYESIMAMA NA KUNYOOSHA MKONO AKIWASALIMIA WANANCHI.

 KATIBU TAWALA WA WILAYA YA KAHAMA TIMOTH NDANYA AKIENDELEA KUWATAMBULISHA WAFANYAKAZI WA MRADI WA TUIMARISHE AFYA (HPSS) WALIOKUWA KATIKA MKUTANO HUO.

 MKUTANO WA HADHARA UKIENDELEA KATIKA UWANJA WA MPIRA NYAMILANGANO HALMASHAURI YA USHETU.

 WAFANYAKAZI WA MRADI WA TUIMARISHE AFYA WAKISILIZA KWA MAKINI HOTUBA YA MKUU WA MKOA.

 BAADHI YA WANANCHI WALIOJITOKEZA KUJIANDIKISHA KATIKA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF ILIYOBORESHWA WAKIENDELEA KUANDIKISHWA.


 

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News