Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WASIOFAHAMIKA WAVUNJA MUZIKI WA KAMPENI ZA CHADEMA DAR


Watu wasiofahamika wamevamia na kuvunja vifaa vya muziki vilivyopangwa kutumika katika mkutano wa kampeni za udiwani wa Kata ya Mbweni wilayani Kinondoni jijini Dar es salaam.
Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akiwa pamoja na Mbunge , Tarime Vijijini John Heche na Mbunge wa Kawe Halima Mdee amesema tukio hilo limetokea leo Novemba 24, 2017  saa 9 alasiri katika uwanja wa Mbweni Vijijini.
Jacob ambaye pia ni diwani wa Kata ya Ubungo, amesema wakati watu wakiwa pembeni wakisubiri viongozi na wanachama kufika eneo hilo ghafla lililotekea gari ndogo lililobeba vijana hao ambao walishuka na kufanya uharibifu huo.
“Walivunja muziki wote uliokuwa uwanjani kisha kuvunja kioo cha gari la matangazo lililokuwa likitumika kuhamasisha watu kuhudhuria mkutano huu,” amesema Jacob.
Amesema hadi sasa bado hawajawatambua watu hao ambao wamefanya uharibifu huo na kwamba, hali ya utulivu imerejea katika eneo baada ya polisi kuwasili na wakati wowote mkutano utaanza wa kumnadi mgombea wao.
Chanzo- Mwananchi.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News