Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MWENYEKITI WA KACU EMMANUEL CHEREHANI APITA BILA KUPINGWA KUONGOZA CHAMA HICHO KWA MUHULA MWINGINE. MWENYEKITI WA KACU EMMANUEL CHEREHANI AKITOA SHUKRANI MARA BAADA YA KUPIGIWA KURA ZA NDIYO KUWA MWENYEKITI.

KAHAMA
Mwenyekiti wa Chama kikuu cha Ushirika KACU Emmanuele Charahan, anaendele  kuwa Mwenyekiti wa chama hicho baada ya  kupita bila kupingwa katika uchaguzi  mkuu wa chama hicho uliofanyika jana mjini Kahama.

Charahani, amechaguliwa tena kuongoza KACU kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo ukiwa ni mhula wake wa pili katika nafasi hiyo ya mwenyekiti ambapo wajumbe wote 210 wa uchaguzi huo walimpitisha kwa kumpigia kura za ndio.

Akizungumza baada ya baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti, Charahani amewashukuru wakulima wa zao la Tumbaku kwa kuendelea kumwamini ili kuwatumikia katika nafasi hiyo na kuomba ushirikianao uendelea ili kufanikisha malengo ya wakulima wa zao hilo hasa katika kuinua uchumi wao.

Aidha aliwataka wakulima wa zao la tumbaku kutokuchanganya  takataka  kwenye kwenye tumbaku kwa lengo la kuongeza uzito kwani hali hiyo inadondoa uaminifu kwa kampuni zinazonunua tumbaku kwa wakulima.

Sambamba na hayo Cherehani amewataka wakulima wa zao la Pamba kuacha kuweka mchanga wa mtoni kwenye pamba zao kwani kufanya hivyo ni kuwapoteza wateja wa zao hilo.

Charahani amewataka wakulima kuendelea kutengeneza mitaji yao wenyewe badala ya kuwa wanategemea mikopo pekee kwani ni njia ya kujiendesha kiuchumi.

Kwa upande wake makamu Mwenyekiti aliyechaguliwa bwana Jofrey Mbuto amesema kuwa atashirikiana na mwenyekiti huyo pamoja na wajumbe wa bodi kuhakikisha wanawatetea wakulima wa mazao ya pamba na Tumbaku pasipo upendeleo.

MATUKIO KATIKA PICHA: 
 
 Wajumbe na wakulima wa zao la Pamba na Tumbaku wakiwa katika ukumbi wa mikutano.
 Wagombea wakiwa mbele ya wapiga kura wakitakiwa kijinadi

 Wagombe wakipita mbele ya wapiga kura wakiwa na namba zao za Ushiriki

 Emmanuel Cherehani aliyeshika kipaza sauti akijinadi na kuomba kura kwa wajumbe
 Mgombea nafasi ya bodi ya wawakilishi Bwana Juma Shilinde akijinadi mbele ya wapiga kura
 Makamu mwenyekiti wa KACU Jofrey Mbuto akijinadi mbele ya wapiga kura.
 Mjumbe wa bodi iliyomaliza muda wake Paul Mayala naye akipokea cheti cha mafunzo hayo.

 Mjumbe wa bodi iliyomaliza muda wake Rashid Ally akipokea cheti cha mafunzo hayo.
 Meneja wa KACU kulia naye akipokea cheti cha mafunz hayo.
 Emmanuel cherehani akipokea Cheti cha mafunzo aliyopitia katika chuo cha ushirika kizumbi
 Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni mwakilishi wa mrajisi kutoka mkoani Dodoma Agustino Senkuruto akitoa ufafanuzi namna ya upigaji kura.
 Mrajisi wa Vyama kutoka mkoa wa Shinyanga akitoa neno kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa KACU.
 Wajumbe wakinyoosha mikono ishara ya kuafiki na kuunga mkono  uuzwaji wa magari ya zamani ya KACU nakununua magari mapya.
 Mkurugenzi wa Uzalishaji na shughuli wa shirika la ununuzi wa Tumbaku Alliance One David Mayunga akitoa maelezo kwa wakulima wa tumbaku kuhusu kuacha kuwatumikisha watoto kwenye mashamba ya Tumbaku pamoja na kutochanganganya maturubai ya blue kwenye Tumbaku.

 Mwakilishi wa Bank ya Azania Prosper Meela akifafanua jambo kuhusu huduma za kibenki kwa wakulima
 Mwakilishi wa benki ya NMB Bwana Elias Tayari akitoa ufafanuzi kuhusu Riba zitolewazo kwa wakulima wa Tumbaku
 Mwakilishi wa benki ya CRDB bwana Juma Mwakalobo akitoa ufafanuzi kuhusu nambna wanavyotoa mikopo kwa wakulima wa Tumbaku
 Wajumbe wa mkutano mkuu wa KACU Wakimsikiliza kwa makini mwenyekiti akitoa maelezo ya nini alichofanya kwa miaka mitatu

 Wajumbe wa KACU wakiwa katika mkutano huo.
 Watumishi wa KACU wakienedelea kupitia maelezo ya mwenyekiti katika kikao hicho.
 Wageni waalikwa na viongozi mbalimbali wakipitia maelezo ya mwenyekiti kuhusu alichokifanya ndani ya miaka mitatu

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News