Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MWANADADA ATEMBEZWA UCHI MBELE YA MAMIA YA WANAKIJIJI,KUFIDIA ADHABU YA KAKA YAKE ALIYEFANYA MAPENZI NA MSICHANA MDOGO.

Mwanadada mmoja katika mji wa Dera Ismail Khan nchini Pakistan ametembezwa uchi wa mnyama mbele ya mamia ya wanakijiji ili kufidia adhabu ya kaka yake aliyezini na msichana mdogo kiumri mwaka 2015.

Taarifa kutoka kwenye gazeti la Tribune la nchini humo zinaeleza kuwa kaka wa msichana huyo aliyetembezwa akiwa uchi, alifanya mapenzi na binti wa familia nyingine hivyo baraza la kijiji liliamuru kaka huyo alipe kiasi cha rupia 150,000 za Pakistan sawa na Tsh milioni 2.2 mwaka jana ili kuyamaliza matatizo hayo kifamilia.

Hata hivyo familia ya Mwanaume huyo mzinifu aliyetambulika kwa jina la Sajjad ilishindwa kutoa fedha hizo ndipo baraza hilo la kijiji lijulikanalo kama (Panchayati) lilipotoa hukumu hiyo ya kumtembeza dada wa Sajjad uchi wa mnyama mbele ya wanakijiji ili liwe funzo kwa familia nyingine.

Tayari polisi nchini Pakistan wametangaza kuwakamata watu saba kufuatia tukio hilo la udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia, wengi wa waliokamatwa ni viongozi wa baraza la kijiji waliotoa hukumu hiyo.

Matukio kama hayo sio mageni nchini Pakistan hii kutokana na msimamo na maamuzi makali ya mabaraza ya vijiji nchini humo kuwakandamiza wanawake.

Mwaka 2002 kulitokea hukumu ya ajabu kama hiyo ambapo mwanamke mmoja ajulikanae kwa jina la Mukhtar Mai aliamriwa kubakwa na kundi la vijana ingawaje alienda kutoa taarifa mapema Polisi.

Mabaraza ya vijiji nchini humo yamekuwa yakitumika kusuluhisha kesi mbalimbali kwenye jamii huku yakilaumu kuwa mahakama nchini humo ni dhaifu katika utendaji ingawaje serikali nchini pakistani haitambui uwepo wa mabaraza hayo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News