Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE KWEMA SEKONDARI KAHAMA WAONYWA KUJIUNGA NA MAKUNDI HATARISHI.MKURUGENZI WA  SHULE ZA KWEMA  POLINE MATHAYO AKIZUNGUMZA KATIKA MAHAFALI HAYOKAHAMA:
Wanafunzi wanaomaliza elimu ya sekondari wametakiwa kutojiunga na makundi hatarishi ambayo yanaweza kuchangia kutofikia Ndoto zao na badala yake wawe na mwenendo bora utakaowawezesha kufikia malengo yao kielimu.

Kauli hiyo imetolewa jana na Meneja wa bank ya DTB, Tawi la kahama MERCY ELIZABETH STEPHEN ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Mahafali ya Nne ya kidato cha nne ya Kwema Modern sekondari School iliyopo mjini Kahama.

MERCY amesema tabia walizonazo na Miendendo yao inatakiwa kuwa kielelezo tosha katika jamii ambapo itawasaidia kuweza kufikia kile ambacho wanakitamani kukipata katika maisha yao

Kwa upande wake Mkurugenzi wa  shule hiyo POLINE MATHAYO amesema wazazi  wanalojukumu kubwa la kuhakikisha watoto wote waliomaliza shule wanaendelezwa kielimu  kwani Ndio urithi pekee uliobaki ambao hawezi kunyang’anywa.

Jumla ya wanafunzi 177  wamehitimu elimu ya sekondari katika shule hiyo, ambao wameahidi kufanya vizuri na kuendelea na Masomo ya juu.

MATUKIO KATIKA PICHA:


MEZA KUU IKIWA IMESIMAMA KUWAPOKEA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE AMBAO WALIKUWA WAKIINGIA UKIMBINI.

WAHITIMU WA KIKE WA KIDATO CHA NNE WAKIINGIA UKUMBINI KWA MADAHA.

WAHITIMU WA KIUME WA KIDATO CHA NNE NAO WAKIINGIA UKUMBINI.

WAHITIMU WOTE KWA PAMOJA WAKITOA SHOW MBELE YA MGENI RASMI HAYUPO PICHANI.

WAHITIMU WAKIENDELEA KUJIMWAYAMWAYA JUKWAANI.

WANAFUNZI WA KIDATO CHA TATU,CHA PILI NA CHA KWANZA WAKIWA NA NYUSO ZA HUZUNI WAKATI KAKA NA DADA ZAO KIDATO CHA NNE WAKIIMBA NA KUCHEZA JUKWAANI ISHARA YA KUAGANA.

MKURUGENZI WA SHULE ZA KWEMA ALIYESIMAMA AKITABULISHA MEZA KUU,MKONO WA KULIA NI MKE WA MKURUGENZI

MKURUGENZI WA SHULE ZA KWEMA MT MATHAYO AKIIMBA BONGO FLEVA NA VIJANA WA KIDATO CHA NNE.

MKURUGENZI WA SHULE ZA KWEMA UZALENDO UKAMSHINDA HAKUISHIA KUIMBA TU HAPA AKIIMBA NA KUCHEZA NA WAHITIMU.

KWEMA NI SHULE YENYA VIJANA WENGI WENYE VIPAJI,HAPA MABINTI WAKIONYESHA UWEZO WAO WA KUCHEZA.

MKURUGENZI WA KWEMA MR MATHAYO AKIMTUNZA MMOJA WA WAHITIMU ALIYEKUWA ANAIMBA WIMBO ALIOUTUNGA YEYE UNAOHUSU SHULE YA KWEMA.

WANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI WAKIONYESHA MCHEZO WA HESABU MBELE YA MEZA KUU.

MKURUGENZI WA SHULE ZA KWEMA AKICHEZA MCHEZO WA HESABU KWA KUKARIRI NAMBA AMBAZO WANAFUNZI HAWAZIJUI  KISHA WANAMTAJIA NAMBA YAKE.

MMOJA WA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE AKIONYESHA UWEZO WAKE KATIKA KUELEZEA MFUMO WA JUA NA NAMNA DUNIA NA SAYARI NYINGINE ZINAVYOFANYA KAZI.

WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE WAKIMKABIDHI MKE WA MKURUGENZI WA SHULE ZA KWEMA TUZO YA KUKUBALI MALEZI WALIYOPATA.

MR AND MRS MATHAYO WAKIPOKEA TUZO YA HESHIMA WALIYOTUNUKIWA NA WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News