Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

LEMMA: CCM KUWACHUKUA WANACHAMA WAKE NI KUSAIDIA KUWAONDOA WAVULANA KWENYE MAPAMBANO.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kwamba kisasi cha CCM kuchukua wanachama wake kitasaidia kuwaondoa wavulana kwenye mapambano ya siasa za upinzani.

Lema ameyasema hayo ikiwa ni muda mfupi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Patrobas Katambi kuomba kuomba ridhaa ya kuingia ndani ya Chama cha Mapinduzi leo katika kikao cha halmashauri Taifa.

Lema amesema kwamba CCM imekuwa na kisasi kikubwa baada ya aliyekuwa Waziri wa Maliasili mstaafu na Mbunge wa Singida Kaskazini  Lazaro Nyalandu kuondoka CCM

"Baada ya Lazaro kuondoka CCM , CCM wamekuwa na kisasi kikubwa , ambacho kimsingi kitasaidia kuondoa wavulana ktk mapambano haya , bado Mameya wawili ? Na kijana mwingine aliyekuwa shupavu 2010-2015. Msiogope kwani wanawaogopa sana na ndio sababu ya matendo haya" Lema.

Kwa upande wa Katibu Mkuu wa Chama hicho Dr. Vicent Mashinji amesema kwamba "Ni muda wa kutofautisha kati ya wanaume na wavulana! wana CHADEMA msihofu tunazidi kuimarika. Kila abiria atashuka kwenye kituo chake lakini safari ya ukombozi inaendelea".

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News