Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

KACU WAZISHUKIA BENKI YA CRDB NA NMB KAHAMA KWA KUCHELEWA KUTOA MIKOPO KWA WAKULIMA WA TUMBAKU. MWENYEKITI WA KACU EMMANUEL CHEREHANI

KAHAMA
 
TAASISI za kibenki zinazotoa mikopo kwa wakulima wa Tumbaku wilayani Kahama mkoani Shinyanga zimetakiwa kutoa mikopo kwa wakati ili kuendana na kalenda ya msimu wa kilimo cha  tumbaku hali itakayosaidia wakulima kuandaa mashamba, kulima na kuvuna kwa wakati.

Wito huo umetolewa leo na Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika  KACU EMMANUEL CHEREHANI wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji wa Mwenyekiti kwa miaka mitatu aliyokuwa madarakani.

CHEREHANI amesema ucheleweshwaji wa mikopo kwenye benk ya NMB na CRDB kwa vyama vya msingi inayosababisha wakulima kushindwa  kufikia malengo ya uzalishai wa zao la Tumbaku.

Aidha CHEREHANI amezihakikishia taasisi za kifedha zinazotoa mikopo kwa wakulima kuwa pesa zao ziko salama na kwamba KACU kwa kushirikiana na vyama vya msingi zitarejesha kwa wakati pesa hizo na hakuna chama hata kimoja kitakachoshindwa kurejesha.

Wakitoa ufafanuzi kuhusu kuchelewa huo, Afisa wa benki ya CRDB JUMA MWAKALOBO na afisa mikopo ya biashara ya Kilimo bank ya NMB Elias Tayari wamesema hali hiyo inatokana na  maombi kutoka  vyama vya msingi kuchelewa kuzifikia benk hizo.

Naye Mkurugenzi wa Uzalishaji na Shughuli wa Shirika la ununuzi wa Tumbaku Aliiance One DAVID MAYUNGA amesema ili kuendeleza zao la Tumbaku nchini wakulima wanatakiwa kupanda miti na kutumia majiko ya kisasa yanayotumia kuni chache na kutowatumikisha watoto.
 MKURUGENZI WA UZALISHAJI NA SHUGHULI WA SHIRIKA LA UNUNUZI WA TUMBAKU ALIIANCE ONE DAVID MAYUNGA


 Mkutano huo, umeambatana na Uchaguzi mkuu wa KACU ambapo mwenyekiti  anayemaliza muda wake EMANULE CHELEHAN amepita bila kupingwa kwa kupata kura zote za ndio 210 huku makamu wake akiwa ni  GEOFREY MBUTO.
 MWAKILISHI WA BANK YA NMB ELIAS TAYARI AKITOA MAJIBU KUHUSU KUCHELEWESHA KUTOA MIKOPO KWA WAKULIMA
 MWAKILISHI WA BANK YA CRDB  JUMA MWAKALOBO AKITOA MAJIBU KUHUSU KUCHELEWESHA KUTOA MIKOPO KWA WAKULIMA

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News