Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

DC KAHAMA AZINDUA RASMI CHUO CHA SAYANSI YA AFYA,DR SHIKA AACHA NEEMA YA MABILIONI KWA YATIMA.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA FADHIL NKURLU KULIA AKITETA JAMBO NA MKURUGENZI WA CHUO CHA SAYANSI YA AFYA NDUGU YONAH BAKUNGILE.
 KAHAMA
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu leo amezidua rasmi chuo cha Sayansi ya afya  kilichopo  Mjini Kahama  ambapo uzinduzi huo umeambatana na  mahafali ya kwanza ya wahitimu wa mafunzo hayo katika Chuo hicho.

Akizungumza  katika Mahafali hayo Nkurlu amewataka wahitimu  wa Fani mbalimbali Wilayani Kahama kuwa waadilifu pale wanapopata nafasi ya kuihudumua jamii ili kukidhi matakwa ya kusomea fani hizo.

NKURLU amesema kuwa baadhi ya wahitimu wa mafunzo mbali mbali wamekuwa wakishindwa kukidhi vigezo kutokana na kutokuwa na nia ya dhati ya kutekeleza wajibu wao kwa weledi na uadilifu.

Akizungumza katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na Wageni mbalimbalu kutoka ndani na nje ya Kahama, Mkurugenzi wa chuo hicho,  YONAH BAKUNGILE amesema baadhi ya Wahitimu wa vyuo vya uuguzi wanakosa uadilifu na kuweka mbele maslahi binafsi hulka inayopoteza maana halisi ya fani hiyo.

Amewataka kuitumikia jamii bila ubaguzi na kuangalia maslahi binafsi ili kwenda sanjari na matakwa na viapo vya kada ya uuguzi duniani.

Katika Mahafali hayo ya kwanza, Jumla ya Wahitimu 33 wametunukiwa cheti cha Msingi katika Kozi ya Mwaka mmoja ya Ufamasia.

Chuo cha Sayansi ya Afya Kahama kilianzishwa mwaka 2016 kikitoa mafunzo katika fani za Ufamasia na Utabibu na kwamba jumla ya wanachuo 33 wamehitimu leo.

Kivutio kikuu katika sherehe hizo ni Dkt LOUIS SHIKA ambaye hivi karibuni amejingea umaarufu, alipojitokeza katika mnada wa nyumba za kifahari za Bilionea SAIDI LUGUMI zilizoko jijini Dar es salaam, kupitia msemo wake wa “(900 INAPENDEZA)” ambapo katika mahafali hayo amehaidi kutoa Bilioni mbili kila mwaka kusomesha watoto yatima katika wilaya ya Kahama.

MATUKIO KATIKA PICHA: Mwanachuo wa Chuo cha Sayansi ya Afya akionyesha Burudani ya Kucheza nyimbo za utamaduni wa kisukuma katika mahafali hayo.

 Mwanachuo akiendelea kutoa Burudani katika Uzinduzi wa chuo hicho.

 Wahitimu wakiingia ukumbini katika mahafali ya kwanza ya chuo hicho.
 Kikundi cha Sanaa kutoka hospitali ya wilaya ya Kahama wakitoa burudani katika uzinduzi huo wa chuo.

 Wahitimu wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiingia kwa furaha wakiwa na Furaha tele.
 Wahitimu wakiwa wameketi katika nafasi zao wakimsubiri mgeni rasmi kuingia ukumbini.

 Mwenyekiti wa mtaa wa Nyasubi Lenard Mayala kulia akiwa na Dr Louis Shika katika sherehe hizo
 Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurulu akikakugua maabara ya kufundishia kwa vitendo katika Chuo hicho.

 Mkuu wa wilaya ya Kahama akiendelea kupata Maelekezo Kuhusu elimu ya vitendo wanayoipata wanachuo katika chuo hicho.
Msafara wa Mkuu wa wilaya ukikagua Chumba cha Computer katika chuo hicho.

Elimu bora ni pamoja na Mazingira bora ya kusomea na kufundishia,Hili ni moja ya darasa katika chuo cha Sayansi ya afya kahama.

Masomo kwa vitendo,Hili ni moja ya darasa la kufundishia likiwa na vifaa vya kisasa vya kufundishia katika chuo hicho.

Masomo kwa Vitendo hiki ni chumba maalumu cha kufundishia kikiwa na mfano wa wodi ambapo wanafunzi wanafundishwa kwa vitendo namna ya kuhudumia wagonjwa wakiwa chuoni hapo.

Moja ya darasa la kufundishia katika chuo cha Sayansi ya afya kilichozinduliwa leo mjini Kahama.

Mkuu wa wilaya akiwa na mkurugenzi wa Chuo hicho pamoja na mke wa mkurugenzi Mrs Bakungile.

Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili katika mahafali hayo.

Familia na Ndugu a Mkurugenzi wa Chuo hicho wakiwa katika sherehe hizo wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni Rasmi

Mkurugenzi wa Chuo cha Sayansi ya Afya Ndugu Yonah Bakungile akitoa neno kwa wahitimu katika mahafali hayo

Wageni waarikwa pamoja na wazazi wakiwa katika sherehe za mahafali na uzinduzi wa chuo cha sayansi ya afya.
Meza kuu ikifuatilia kwa makini burudani ya nyimbo za asili.

Mwenyekiti wa bodi ya shule akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Kahama kutoa Hotuba yake.

Mkuu wa wilaya ya kahama akitoa hutuba kwa wazazi na wahitimu katika mahafali hayo.\

Mgeni muhimu wa katika mahafali hayo Dr Louis Shika akipeana mkono na wageni wa meza kuu baada ya kutoa neno lake.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mjini Kahama wakiwa katika sherehe hizo.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News