Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

ACACIA BULYANHULU YAIPA HALMASHAURI YA MSALALA ZAIDI YA BILIONI MOJA KWA AJILI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BUGARAMA.

KAIMU MENEJA WA MGODI WA ACACIA BULYANHULU ELIAS KASITILA MWENYE MIWANI AKIMKABIDHI MKATABA WA MAKUBALIANO YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BUGARAMA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MSALALA MIBAKO MABUBU.

KAHAMA.

Kampuni ya Acacia Kupitia mgodi wa Dhahabu wa Bulyanhulu Leo imesaini mkataba wa Shilingi Bilioni Moja  na milioni mia moja themanni na tisa na Halmashauri ya Msalala Wilayani Kahama kwa ajili ya Ujenzi wa awamu ya Pili wa kituo Cha Afya cha Bugarama kilichopo Kakola wilayani Humo.

Akizungumza kabla ya kusaini mkataba wa msaada huo leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa  Halmashauri hiyo, ZABLON DONGE azitaka kampuni za KASHERE ENTERPRISES LTD na HIGEN CONSTRUCTION CO LTD zinazotekeleza mradi huo kuutekeleza kwa wakati na kwa kiwango.

Naye Kaimu Meneja Mkuu wa mgodi wa Acacia Bulyanhulu, ELIAS KASITILA amesema mgodi umefadhili awamu ya kwanza na ya pili ya ujenzi wa kituo hicho cha afya ikiwa ni kurudisha fadhila kwa jamii inayozunguka mgodi kwa kile walichokipata.

Sambamba na hayo Kasitila ametoa wito kwa wakandarasi kutoa nafasi za kazi za vibarua kwa wazawa wa eneo hilo na siyo kutoa vibarua nje ya halmashauri ya msalala.

Kwa upande wake, mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya HIGEN CONSTRUCTION CO LTD moja ya kampuni zilizopewa zabuni ya ujenzi wa kituo hicho, THEMISTOCLES RWOTA amesema kampuni yake iko tayari kutekeleza mradi huo kwa uaminifu na ufanisi mkubwa. 

Ujenzi wa kituo cha afya Bugarama ni maandalizi ya kukifanya kituo hicho kuwa hospitali ya wilaya ya Msalala kwa mujibu wa maelekezo ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, UMMY MWALIMU alipotembelea kituo hicho mapema mwaka huu.

Katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi huo, Mgodi wa Acacia Bulyanhulu umetoa kiasi cha dola za Marekani laki nne na themanini na tano elfu ambazo ni sawa na shilingi bilioni moja na milioni tisini.

MATUKIO KATIKA PICHA:


 KAIMU MENEJA WA MGODI WA BULYANHULU ELIAS KASITILA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI NJE YA UKUMBI WA HALMASHAURI YA MSALALA BAADA YA KUSAINISHANA MIKATABA.

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MSALALA MIBAKO MABUBU KUSHOTO AKIMKABIDHI MIKATABA YA MAKUBALIANO KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MSALALA ZABRON DONGE.

 WAKURUGENZI WA KAMPUNI YA KASHERE ENTERPRISES LTD na HIGEN CONSTRUCTION CO LTD WALIOSHINDA ZABUNI YA UJENZI HUO WAKISAINI MIKATABA WA KUKUBALI KUFANYA KAZI YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA BUGARAMA.

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MSALALA MIBAKO MABUBU KUSHOTO AKIMKABIDHI MIKATABA YA UJENZI HUO MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HIGEN CONSTRUCTION CO LTD BWANA THEMISTOCLES RWOTA

 MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MSALALA MIBAKO MABUBUAKISAINI MKATABA WA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BUGARAMA.

 MKURUGENZI WA KAMPUNI YA HIGEN CONSTRUCTION CO LTD BWANA THEMISTOCLES RWOTA AKIELEZA NAMNA WATAKAVYOFANYA KAZI NA KUMALIZA KWA WAKATI NA AMEHAIDI KUWATUMIA VIBARUA WA ENEO HUSIKA LA MRADI/

 WAKURUGENZI WA KAMPUNI WATAKAOJENGA KITUO CHA AFYA WAKIWA KATIKA OFISI ZA MKURUGENZI WA HALMSHAURI YA MSALALA AMBAPO MIKATABA HIYO IMESAINIWA.

 MWANASHERIA WA HALMASHAURI YA MSALALA KUSHOTO AKIWA NA MGANGA MKUU WA HALMASHAURI YA MSALALA WAKIFUATILIA NA KUSOMA KWA MAKINI MIKATABA YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BUGARAMA.

 KAIMU MENEJA WA MGODI WA BULYANHULU ELIAS KASITILA AKIZUNGUMZA KATIKA OFISI ZA MKURUGENZI WA HALMSHAURI WA MSALALA KUHUSU NAMNA WATAKAVYOTEKELEZA MRADI HUO.

 MIKATABA IKIWA MEZANI KABLA YA KUSAINIWA 

 WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU WAKIWA KATIKA OFISI ZA MKURUGENZI WAKATI WA ZOEZI LA KUWEKEANA SAINI MIKATABA YA UJENZI WA KITUO CHA AFYA BUGARAMA.

 KAIMU MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MSALALA ZABRON DONGE AKISISITIZA JAMBAO MARA BAADA YA KUSAINIWA KWA MIKATABA HIYO.

 KAIMU MENEJA WA MGODI WA BULYANHULU ELIAS KASITILA ALIYESIMAMA AKISISITIZA JAMBO KWA WAKANDARASI KUHUSU KUTOA AJIRA KWA WAZAWA WAKATI MRADI UTAKAPOANZA

KAIMU MENEJA WA MGODI WA BULYANHULU ELIAS KASITILA KATIKATI AKIWA NA WAKURUGENZI WA KAMPUNI ZA KASHERE ENTERPRISES LTD na HIGEN CONSTRUCTION CO LTD WATAKAOJENGA KITUO CHA AFYA CHA BUGARAMA.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News