Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania

Tunakushukuru Sana kwa kuwa sehemu ya Mtandao wetu kwa takriban miaka 10 sasa! Tumesitisha Huduma kwa Muda Mpaka hapo Baadaye!

COPYRIGHT © Kijukuu Cha Bibi K | Habari,Matukio na Burudani Tanzania | POWERED BY ZOTEKALI WEB SERVICES

#Blog visitors

Kumbukumbu za Habari

POKEA HABARI KWA EMAIL

#Blog Tags

Ad Home

Header Ads

#All Popular News

Kijukuu Online Tv

Sikiliza KAHAMA FM

Advertisement

Banner

kijukuu-banner

MDEE AMTAHADHARISHA NYALANDU KUHUSU CHADEMA

Mbunge wa Kawe jijini Dar es salaam, Halima Mdee amemkaribisha na kumtahadharisha aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akimtaka ajiandae kisaikolojia kupambana na changamoto wanazokumbana nazo viongozi wa Chadema.

Ameyasema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii wa Twitter kumkaribisha ndani ya chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mara baada ya kutangaza kukihama Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiuzulu nafasi ya Ubunge.

“Mhe. Nyalandu karibu sana CHADEMA. Naamini utakuwa imara kukabiliana na siasa za chuki, ubaguzi na visasi zinazolikabili taifa letu, hivyo naimani umechukua maamuzi mazuri ila jiandae kukabiliana na changamoto,”amesema Mdee

Jana  Nyalandu ambaye alikuwa Mbunge wa Singida Kaskazini na Mjumbe wa Halmashauri ya Kamati  Kuu CCM alitangaza kujiuzulu nafasi zake hizo kwa kile alichodai kwamba hafurahishwi na mambo ya kisiasa yanayoendelea nchini na kuwaomba wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kama wataridhia wampe nafasi ili kuweza kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi kupitia chama hicho.

No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!

#Weekly Top News