Header Ads

MATUKIO YA AJALI YA BASI LA WIBONELA MJINI KAHAMA.

HII NDIVYO HALI ILIVYOKUWA YA BASI HILO.

KAHAMA.
Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine arobaini kujeruhiwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga baada ya kutokea ajari mbaya iliyohusha basi la abiri.

Tukioa hilo lilitokea jana majira ya saa Kumi na mbili asubuhi katika eneo la Phantom Nje Kidogo mwa mji wa Kahama,wakati basi aina ya Scania lenye no T 412 CGN mali ya Wibonela Ambalo lilikuwa likitokea mjini Kahama kwenda jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka.

Kwa mjibu wa Mganga Mfawidhiwa Hospitali ya mji wa Kahama Joseph Ngowi alisema walikufa kati yao wanaume ni 3 akiwemo mtoto na mwamke ni Mmoja ambapo aliataja kuwa ni Amina Emmanuel ambaye alikuwa mjamzito mkazi wa Kigoma, Salum ambaye alifahamika kwa jina moja , Mtoto wa miezi mitatu Robin Jordan na mwanamme mmoja mabaye hakufahamika.

Aliataja waliojeruhiwa ni Mauld Shaban (44) mkazi wa Ushirombo, Athuman Issa (21) mkazi wa Kahama, Jordan Mbeya (28) mkazi wa Kasulu, Brandina Patrick (24) mkazi wa Kasulu, Oscar Lameck (19) Mkazi wa Kigoma, Stamili Shaban (38) mkazi wa Dodoma, Neema Dastan (18) Mkazi wa Kahama na Monica Gadson (35) mkazi wa Kahama.

Wengine ni Nickson Andati ambaye ni Mchungaji amkazi wa Nchi ya Rwanda (34) Lucas Mlezi (48), Joyce Fred (28) Asnati Remtula (27) , Eveline Hamis (6), Happy Hamis (30), Japhet Masha (29), Jackson Elisanto (26), Buligelila Ramadhadhan (40) na Lita Bryson (25) wote wakazi wa Kahama.

Irene Wilson (17) mkazi wa Kasulu, John Lembo(45) Mkazi wa Bariadi, Hamis Shaban (31) mkazi wa Kahama, Emmanuel Lambambo (32) mkazi wa Kigoma, Kashindye Masanja (28), Frenk Kishimba (21) Peter Bahati (22) wote wakazi wa Kahama, Iseme Ilila (36) mkazi wa Katoro Geita, Ebrania Saga (30) mkazi wa Kigoma, na Anika Amdani (35) Mkazi wa Kahama.

Wengine ni Shaban Omary (16) amabye ni Mkazi wa Dodoma,Grolia Moses (18) mkazi wa Kahama, Agnesi Broto (35) Mkazi wa Ngara, Kulwa Said (40) mkazi wa Kahama, Peter David (42) mkazi wa Kahama,Tunga Lazaro (22) mkazi wa Mariadi, na Happy David (32) huku majeruhi wengine wakishindwakutambulika kutokana nakuwa mahututu.

Shuhuda wa Tukio hilo Isemi Ikili ambaye alikuwa abiria alisema chanzo cha ajali  hiyo   ni dereva wa basi hilo kuendesha mwendokasi wakati akitoka Katika kituo kikuu cha mabasi huku ikielezwa kwamba alikuwa akifukuzia mabasi yaliyotangulia ambapo inadaiwa alikuwa anawahi kwenye Mzani uliopo Mwendakulima wilayani Hapa.

Alisema walipofika kwenye kona ya kutoka Mjini Kahama Kuelekea Isaka dereva ilimshinda ndipoa liporuka ambapo na kuangukia katika Mtaro na kupinduka vibaya.

Majeruhi mwingine aliyezungumza na  nipashe ,Peter Bahati alisema kabla ya kutokea kwa ajali hiyo abiria walikuwa wakimlalamikia dereva kutokana na mwendokasi alikokuwa nao wakati wa kuondoka Kituo cha mabasi ambapo dereva baada ya kuona inamshinda.

Mili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwaajili ndugu na jamaa kufika kutambua ndugu zao huku majeruhi wakiendelea kupatiwa matibabu na mahututi wanantarajiwa kupatiwa Rufani kupelekwa katika hospitali za rufaa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha alifika katika tukio hilo ambapo alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa Tukio Hilo.

MATUKIO KATIKA PICHA:

Ule msemo wa kufa kufaana umemponza kijana huyu aliyekuwa anawaibia abiria waliopata ajali hapa ni baada ya kukamatwa na wananchi wenye hasira kali na kumpiga kiberiti.
Hivi ndivyo ilivyokuwa katika ajali hiyo
 Naye aliandikiwa kufa hivi mungu amrehemu.
 Umati mkubwa wa wakazi wa eneo la Phantom wakishundia basi hilo lipopinduka leo asubuhi . Hivi hali halisi ya ajali ya basi la wibonela lipopata ajali mjini kahama .
 baadhi ya viti vya basi hilo vikiwa vimetoka kambisa takiribani nusu ya basi hilo .
 Baadhi ya askari polisi  wakiwa eneo la tukio ili kuzui wizi wa aina yonyote katika eneo hilo la ajali .
 Haya ndiyo mabaki ya basi ilipopata ajali lla wibonela asubuhi ya leo mjini kahama .
 Basi la wibonela likiwa limeruka mtalo mkubwa katika eneo la phantom mjini kahama hivi leo asubuhi .
 Hali ya basi hilo ndiyo lilivyokuwa minguu yake juu baada ya kupata hajari hivyo asubuhi .
  Baadhi la rai wema wakijaribu kutoa msandaa kwa majeruhi wa basi hilo .

 Baadhi ya wakazi wa nyasubi wakiangalia basi la wibonela livyoruka mtalo huu mkubwa .
 Majeruhi wa basi la wibonela wakiwa hospitali ya wilaya kahama kwa matibabu zaidi .
 Hii ndiyo kona ilivyomsinda dereva wa basi hilo la wibonela leo katika eneo la phantom
 Askali wa usalama barabarani akihojiana na majeruhi katika hospitali ya wilaya ya kahama .
 kila moja alishangaa basi hilo livyopita mtalo huu mkubwa .
 Baadhi ya majeruhi wakiwa wodi  namba 8 katika hospital ya wilaya ya kahama.
 Mmoja wa majeruhi wa basi la wibonela Emmanuel lambambo mkazi wa  kasulu kigoma  akiwa amejeruhiwa eneo la kichwa .
 Baadhi ya majeruhi wakiwa wamejeruhi vimbaya sehemu za mili yao . .
 Moja wa majeruhi oscar lameck akiwa tabani hospitali .

 Majeruhi wakiwa hoi  katika wodi namba 8 akiwa na majeraha sehemu ya kichwani .
 Majeruhi wakiwa hoi hospitali ya wilaya kahama  baada ya kupata huduma akiwa ajapata fahamu  .
 Baadhi ya wananchi wa kahama wakijaribu kuangalia jamaa zao walipata ajali katika wodi namba 8.
 Majeruhi wakiwa wodini  namba nane 8 katika hospital ya wilaya kahama .
 Majeruhi wa minguu ambapo mguu wake wa kulia humevujika.
 Baadha ya majeruhi  maulidi shabani   akiwasiliana na  ndugu zake hospital kahama
.
 Kati ya watu wanne walifariki akimwemo mtoto moja wa miezi mitatu wakiwa wameifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospital ya wilaya huku mama yake mzazi akiwa majeruhi .
 Majeruhi wa basi la wibonela akiwa hoi huku akiwa na majeaha makubwa katika kichwa chake .
 Baadhi njamaa wakijaribu kuwatabuha majeruhi au ndugu zao hospital ya wilaya kahama .
Majeruhi wakiwa chini na baadhi watu wakiwangali na kuwatabuha njama zao.


No comments

Karibu tena,asante kwa kusoma habari hii!